Sheria na Masharti

1. KWA UJUMLA

SBT CO., LTD. (SBT) huendesha tovuti www.sbtjapan.com (tovuti) kwa mujibu wa Masharti ya utumiaji yafuatayo. Kwa kutumia tovuti, unakubaliana kuwa unakubali masharti haya.

2. HAKI MILIKI

Hakimiliki kwa yote yaliyomo kwenye tovuti ni ya SBT. Matumizi na chombo kingine kwa yale yaliyomo kwenye tovuti ni marufuku.

3. MAKUBALIANO MENGINE

Masharti haya yanasimamia matumizi ya tovuti. MASHARTI YA BIASHARA ya SBT ndiyo yanayotambulika kusimamia shughuli zote isipokuwa pale ambapo SBT itasaini mkataba tofauti wa maandishi nawewe.

4. MASHARTI YASIYO YA KIINGEREZA

Toleo la Kiingereza la maneno haya pekee ndilo linaloidhinishwa. Tafsiri zisizo za Kiingereza hazitumiki kwenye mwongozo wa kazi na zinakusudiwa tu kwa ajili ya kutoa urahisi kwa mhusika.

5. USAJILI

Kusajili akaunti ya mteja wa SBT inahitajika ili kufanya miamala. Usajili ni bure. Ili kujisajili, ni lazima utoe taarifa zako na SBT za sasa ambzazo ni sahihi na kamili. SBT haitawajibika kwa hasara inayotokana na taarifa zisizo sahihi. Baada ya kupokea kitambulisho cha kuingia, unaweza kutazama bei na kufanya miamala.

6. MIAMALA

Miamala inasimamiwa na MASHARTI YA BIASHARA yaliyotolewa pamoja na ankara. Bidhaa kwenye tovuti zinauzwa kwa sarafu za EUR, GBP, JPY, au USD na, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo kwa maandishi, hutolewa kwa bei ya manunuzi na usfiri au manunuzi bila usafiri. SBT inakubali malipo katika sarafu iliyotajwa kwenye ankara pekee. Gharama za benki na gharama zingine za muamala hazijajumuishwa kwenye bei ya ankara na zinatakiwa kulipwa na wewe.

7. YALIYOMO KWENYE TOVUTI

SBT hufanya uangalifu unaostahili katika kuchapisha habari kwenye tovuti; hata hivyo, SBT haitoi dhamana ya ukamilifu, usahihi, uhalali, usalama, au usasishaji wake. SBT haitawajibika kwa hasara inayotokana na maamuzi au hatua zilizochukuliwa na wewe kutegemea taarifa za kwenye tovuti.

8. WARANT NA UWAJIBIKAJI

SBT inatoa tovuti na yaliyomo kama yalivyo. Kwa kiwango cha juu kinachoruhusiwa na sheria, SBT haitoi waranti hata ile ya kudokezwa kuhusiana na kutumia, kutokuwa na uwezo wa kutumia, au matokeo ya kutumia tovuti na yaliyomo ndani yake, na haiwajibiki kwa uharibifu utakaojitokeza, usio wa moja kwa moja, au wa adhabu kutokana na kupoteza biashara, faida au matumizi.

9. MATUMIZI MABOVU

Matumizi mabaya yanajumuisha, lakini sio tu, kuunda akaunti nyingi au za ulaghai za wateja wa SBT; kukiuka sheria inayotumika, kukiuka masharti haya, au sera zilizoandikwa za SBT; na vitendo vingine vya ulaghai au nia mbaya. SBT inaweza kusimamisha au kughairi akaunti dhuluma za mteja wa SBT bila notisi. Unatahadharishwa kwamba utafidia SBT kwa hasara inayotokana na ukiukaji wako wa masharti haya, uzembe, makosa, au ukiukaji wa mkataba au haki au sheria za watu wengine.

10. UTUNZAJI WA DATA

SBT inatii Sheria ya Japani ya Ulinzi wa Taarifa binafsi, Sheria ya Matumizi ya Mfumo wa Usalama wa Jamii na Nambari ya Kodi, na sheria nyingine zinazotumika za kushughulikia data. Vilevile hushughulikia data ya mada kulingana na Sera ya Faragha ya SBT inayopatikana katika www.sbtjapan.com/privacypolicy.

11. KUPINGA UFISADI

SBT inatii Sheria ya Japani ya Kuzuia Ushindani Usio na Haki, Mkataba wa OECD wa Kupambana na Utoaji Hongo wa Maafisa wa Kigeni, na sheria zingine zinazotumika dhidi ya ufisadi. Muamala wowote unaokiuka marufuku.

12. TOFAUTI NA MATAKWA YA JAMII

SBT kamwe haijishughulihi na uhalifu uliopangwa na hudumisha sera za utiifu wa ndani ili kuzuia miamala isiyo halali, ikijumuisha kukagua washirika wa biashara kwa miunganisho isiyo kubalika kijamii na vilevile ikijumuisha masharti ambayo yanazuia matumizi ya nguvu zisizo halali kijamii katika ununuzi na mikataba ya mauzo. Muamala wowote unaokiuka ni marufuku.

13. UDHIBITI WA BIDHAA ZA KIMATAIFA

SBT inatii sheria na kanuni za usalama wa ndani na za kimataifa na kupambana na ugaidi, ikijumuisha vidhibiti vya orodha na vidhibiti vya kukamata vitu vyote vinavyokataza malipo kwa nchi zilizo orodheshwa, watu walio orodheshwa, au kwa bidhaa zilizo orodheshwa, yaani. silaha na vifaa vya nyuklia. Muamala wowote unaokiuka ni marufuku.

14. MENGINEYO

Ukosefu katika kutekeleza au kuhitaji utoshelevu wa utoaji, utendaji, kutokuwepo, hali ya utendaji, au kiwango cha utendaji hautaondoa haki, suluhu au sharti. Ikiwa sehemu ya masharti haya hayatekelezeki, yaliyosalia yataendelea kutumika kama yalivyoandikwa isipokuwa pale ambapo hayawezi kutekelezeka. Masharti haya yanatawaliwa na kuamuliwa na sheria na mahakama za Japani pekee.