Sheria na Masharti

1. JUMLA

SBT CO., LTD. (SBT) huendesha tovuti www.sbtjapan.com (tovuti) kwa mujibu wa sheria na masharti yafuatayo (msharti). Kwa kutumia tovuti, unakiri kuwa unakubali masharti haya.

2. HAKIMILIKI

Hakimiliki kwa maudhui yote yaliyo kwenye tovuti hii ni ya SBT. Uzalishaji upya au utumiaji wa maudhui yaliyo kwenye tovuti hii ni marufuku.

3. MAKUBALIANO MENGINE

Masharti haya yanaongoza miamala yote isipokuwa ambapo SBT inatia sahihi kandarasi tofauti ya maandishi nawe. SBT ikitia sahihi kandarasi nawe, kandarasi hiyo itadumu pale ambapo kandarasi hiyo na masharti haya vintofautiana.

4. MASHARTI YASIYO YA KIINGEREZA

Ni toleo la Kiingereza pekee la masharti haya lililo na mamlaka. Tafsiri ambazo si za Kiingereza zinatumika na kusudiwa kw urahisishaji pekee.

5. USAJILI

Usajili wa akaunti ya mteja unahitajika ili kufanya miamala. Usajili ni wa bila malipo. Ili kujisajili, lazima uipe SBT taarifa sahihi, kamilifu na ya sasa. SBT haitawajibika kwa upoteaji unaotokana na taarifa zisizofaa.

6. UWEKAJI BEI NA MAUZO

Magari yanawekwa bei kwa dola za Marekani au yen ya Japani na, isipokuwa ibainishwe vinginevyo kwa maandishi, kuuzwa kwa masharti ya CFR au FOB.

7. MALIPO

Malipo yote au kiasi yanalipwa siku saba baada ya kutuma ankara na husemekana kulipwa kwa SBT kupokea uhamisho wa hela zako kwa njia ya elektroniki. Kwa magari yanayosafirishwa kwa malipo kiasi, malipo kamili yanahitajika siku saba baada ya tarehe ya usafirishaji wa mtoa huduma. Ada za benki na gharama nyingine za miamala hazijumuiswhi katika bei ya ankara na wewe ndiwe unayelipa.

8. UWASILISHAJI NA USAFIRISHAJI

Baada ya malipo yote au kiasi, SBT inaweka nafasi ya usafirishaji kulingana na masharti ya mtoa huduma. Eneo la kuwasilisha ni kituo cha mtoa huduma. Hatari zinaenda kwako kwa kumlipa mtoa huduma. Ratiba za watoa huduma ni za kukadiria na SBT haitawajibika mtoa huduma akichelewa, akikosea au asipotekeleza kazi. Lazima uzingatie sheria na utaratibu wa uingiza bidhaa , ikiwemo vikwazo vya umri wa wa gari, daraja na upande wa kuendeshea gari. SBT haitawajibika kwa kutozingatia sheria wala kukatazwa kuingia. Baada ya kupokea shehena, SBT inashauri kuangalia na kujaza mafuta ya mtambo, kimiminiko cha kupozea cha rejeta na matumizi mengine.

9. NYARAKA

Nyaraka halisi za usafirishaji zinatolewa na kutumwa kwako tu baada ya malipo yote. Lazima ulipe kwa wakati malipo yote kwa ajili ya uchakataji na kutuma kabla ya kuwasili kwa POD ya shehena. SBT haitawajibika kwa hasara inayotokana na nyaraka zilizoharibika, chelewa, zisizo sahihi, zilizopotea, zisizorekebishwa, zisizowasilishwa wala kuhifadhiwa.

10. KUTOLIPA NA KUGHAIRI

Ukikosa kulipa SBT bei kamili iliyo kwenye ankara kufikia siku saba baada ya tarehe ya usafirishaji wa mtoa huduma, gari litasemekana kutolipwa na huenda ukafutilia mbali malipo yoyote kiasi. SBT ina haki ya kumiliki na inaweza kuuza tena gari ambalo halijalipwa. Baada ya SBT kumpa mtoa huduma gari, agizo haliwezi kughairiwa.

11. MAUDHUI YA TOVUTI

SBT huwa makini inapochapisa taarifa kwenye tovuti; hata hivyo, haitoi uhakikisho wa ukamilifu, usahihi, uhalali wala usalama wake. SBT haitawajibika kwa upoteaji unatokana na maamuzi wala hatua zinazochukuliwa nawe kwa kutegemea taarifa zilizochapishwa kwenye tovuti.

12. WATOA HUDUMA WASIO WASHIRIKA

Unakiri kuwa watoa huduma wasio washirika, ikiwemo benki na wasafirishaji, hawadhibitiwi na wala kuhusiana na SBT na SBT haitawajibika kwa upoteaji unaotokana ana utumiaji wao kwa gari lisilomilikiwa na mhusika mwingine au kwa uchelewaji wa mhusika asiye mshirika, makosa au kutotekeleza.

13. HAKIKISHO

SBT inatoa tovuti na magari na kwa kiwango cha juu kinachoruhusiwa na sheria inakanusha mahakikisho yote, ikiwemo ufaafu kwa madhumuni na uchuuzaji, isipokuwa kwa barua yenye maelezo. SBT inahakikisha tu kuwa magari yanaoana na maelezo yaliyo kwenye tovuti. SBT haitawajibika kwa kasoro za gari zilizofichuliwa.

14. DHIMA YA UKOMO

SBT haitawajibika kwa zaidi ya bei ya ankara ya gari au magari husika; uharibifu unaoandamana na, usio wa moja kwa moja au wa adhabu; au kupoteza biashara, faida au utumiaji.

15. FIDIA BIMA

Utafidia SBT kwa hasara inayotokana na ukiukaji wa masharti haya, uzembe, makosa, au ukiukaji wa kandarasi au haki au sheria ya mhusika mwingine.

16. KUPAMBANA NA UFISADI

SBT inazingatia Sheria ya Kuzuia Ushindani Usio wa Usawa ya Japan, Mkataba wa OECD kuhusu Kupambana na Rushwa ya Maafisa wa Umma wa Kigeni na sheria nyingine inayotumika ya kupambana na ufisadi. Muamala wowote unaovunja sheria ni marufuku.

17. VIKUNDI VYA KUTEKELZA UHALIFU KATIKA JAMII

SBT inadumisha mpango wa ndani wa uzingatiaji ili kuzuia miamala ya uhalifu katika kijamii ambao ni pamoja na kuchunguza washirika wa biashara kwa mashirika ya kutekeleza uhalifu katika jamii na kushirikisha masharti ili kuondoa vikundi vya kutekeleza uhalifu katika jamii kwenye mauzo na kandarasi za ununuzi. Muamala wowote unaovunja sheria ni marufuku.

18. UDHIBITI WA USALAMA WA KIMATAIFA

SBT huzingatia sheria na kanuni za kupambana na ugaidi na usalama wa nyumbani na kimataifa, ikiwemo list controls na catch-all-controls ili kuzuia ueneaji wa WMD. Muamala wowote unaovunja sheria ni marufuku.

19. ZIADA

Masharti haya yanahusisha makubaliano yote kati yako na SBT na uvumilivu wa kutekeleza au kuhitaji uridhikaji wa kipengee, sheria, kutotekeleza, au uelekeo wa kukabiliana hautaondoa haki, suluhisho wala sharti. Ikiwa sehemu ya masharti haya itaonekana isiyoweza kutekelezwa, mengine yote yatatumika kama yalivyoandikwa isipokuwa pale yasipotekelezeka. Masharti haya yanaongozwa na kusimamiwa na sheria na mahakama ya Japan pekee.