Wafanyikazi wetu

Makao yetu makuu yako mjini Yokohama Japani na tunazo afisi 33 za maeneo katika mataifa mbali mbali,SBT CO., LTD. inao wafanyakazi zaidi ya 1000 kote nduniani. Kamwe hatuwezi kulegeza kuwakuza wafanyakazi wetu ili kuhakikisha huduma bora zaidi kwa wateja wetu waaminifu.

Ni vipi tunahakikisha ubora wa huduma zetu?

Kabla ya kusafirisha, magari yote hupitia utaratibu wetu wa kina wa utunzaji. Wafanyakazi wetu wenye uzoefu na ujuzi usafisha kila gari kabla ya kuwa tayari kusafirishwa.

Tunao wataalamu wa kiufundi kwenye mabohari (yadi)yetu. Wanafanya utambuzi mzima wa injini, sehemu zinginezo, usambasaji, na mitambo mingine ya stima kwa kutumia vifaa vya skana vya hivi punde kabisa ili kuthibitisha kuwa kila sehemu ya gari iko katika hali nzuri kabisa.

Mabohari (yadi)yetu yametunzwa vizuri ili kuhifadhi maelfu ya miundo maarufu ya magari kwa wakati mmoja. Tunaweka wafanyakazi wetu kwenye mazingira masafi na ya kuvutia kwa wafanyakazi ili kuwatia motisha wataalamu wetu wenye tajriba na kujitolea, ili wapeane huduma za juu zaidi kwa wateja.

Wanunuzi:

Wafanyakazi wetu wapambanuzi wako katika minada yote mikuu ili kununua magari ya ubora wa hali ya juu. Tunayakagua magari yote kwa umakini kabla ya kuyanunua. Wanaonunua wanayo maarifa mengi kuhusu kuuza nje ya nchi, minada na sekta ya magari yaliyotumika ili kuwapatia wateja wetu thamani ya juu.

Wanaofanyakazi kwa bohari (yadi):

Wafanyakazi wetu walio kwenye bohari (yadi)hutoa huduma za ukaguzi za ziada kwa magari yote kabla ya kusafirishwa. Wanao ujuzi wa kutosha kurekebisha kasoro ndogo ndogo na kuyasafisha magari yote katika bohari (yadi)kabla ya kusafirishwa.

Wafanyakazi wa kitengo cha mauzo:

Wafanyakazi wetu wa kitengo cha mauzo ambao wananena lugha nyingi, wapendao kazi na wenye maarifa mengi kuhusu sekta hutoa huduma bora kabisa kwa wateja masaa ishirini na manne kwa siku kote nduniani.

Wafanyakazi wa utawala:

Wafanyakazi wetu wa ofisini wenye uzoefu ushughilikia nyaraka zote kwa niaba ya wateja ili kuimarisha upokezi Nyaraka wa haraka na wa hakika. Kwa muda mrefu, tumejenga uhusiano mwema na kampuni za uchukuzi wa baharini, zinazotuwezesha kusafirisha magari yako kwa urahisi, bila kupoteza muda na kwa mfululizo.

Wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja:

24/7 Wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja watakusaidia katika awamu yoyote ya ununuzi hadi upokee (ma)gari lako.
Contact us at +81-45-290-9485 au csd@sbtjapan.com