• Nyumbani >
  • FAQ (Maswali tunayoulizwa kwa wingi)

Maulizo

Q. Je, ni nini nahitajika kufanya ili kununua gari?

Usajili unahitajika. Usajili utakapokamiliak, unaweza kununua gari lolote ulitakalo.

Q. Je, mnao utaratibu mnaofuata ili kuwa mshirika aliye sajiliwa na SBT?

Muuza magari yeyote au mnunuzi wa kibinafsi anaweza kujisajilisha kama mshirika. Lakini, kwa mnunuzi wa kibinafsi, tunahimiza adhibitishe kanuni za taifa lake kabla ya kununua. Hatufahamu sheria za taifa lako. Hatuwezi kukupatia mawaidha yoyote, au kupendekeza muuza magari yeyote au (Wakala) dalali wa forodha yeyote aliye nchini mwako.

Q. Je, ni magari mangapi yaliyotumika ambayo yanapatikana kwenye hifadhi zenu na kwenye mnada?

Kwa kawaida, Tunayo zaidi ya magari elfu moja kwenye hifadhi yetu ya kila siku. Zaidi ya hayo, unaweza kuyapata takriban magari 150,000 kwa wiki yaliyo kwenye minada tofauti ya mtandao tunayoshiriki. Kwa kawaida tunazo shehena 2 au 3 za meli za RORO pamoja na 4 au 5 za meli za kontena kila mwezi.

Q. Je, ni malipo ya aina gani yanayokubalika na SBT?

Kwa sababu ya ulaghai wa kila mara wa kadi za mkopo (Credit Card), huwa hatukubali malipo ya kadi za mikopo (Credit Card). Huwa tunakubali malipo ya Telegraphic Transfer (TT) kutoka kwa benki yako hadi kwa akaunti yetu ya benki iliyo orodheshwa.

Q. Je, itanichukua muda gani kupokea gari langu?

Hatuwezi kwa hakika kupatia saa kamili ambazo gari lako litawasili maanake inategemea ratiba ya uchukuzi wa meli. Lakini, gari lako litasafirishwa kwa meli ambayo itakuwa ya kwanza kung'oa nanga.

Q. Kunao ada yoyote ya ushirika?

Hakuna. Hakuna malipo au ada zilizofichwa zinazohitajika. Kwa hivyo usisite na Jisajili sasa.

Q. Iwapo nitanunua gari kwa $2,000, ni pesa ngapi ambazo nitalipa kama gharama ya ziada?

Kama bei ni ya FOB, utahitajika kulipa gharama ya kusafirisha shehena, malipo ya forodhani, ushuru wa kununua bidhaa nje ya nchi, ada ya usajili, ada ya uzingatiaji, na gharama zingine zozote zinazoweza kutokea kulingana na kanuni za taifa lako.
Kama bei ni ya C&F, unaweza kuondoa gharama ya kusafirisha shehena kutoka kwa maelezo yaliyotangulia.

Q. Naweza kununua magari yenye kishikio cha usukani kushoto (LHD) kutoka SBT?

Magari yenye kishikio cha usukani kushoto (LHD)ni nadra sana Japani. Magari yenye kishikio cha usukani kushoto (LHD)kwa kawaida uagizwa kutoka mataifa kama Marekani, Ulaya na Korea. Lakini, unaweza kutafuta magari yenye kishikio cha usukani kushoto (LHD) kwa kiasi cha haja kutoka hifadhi za Korea na Marekani.

Q. Naweza nikafuta agizo langu la ununuzi?

Ukifuta agizo, tunaweza kuhitajika kuliuza gari hilo tena kwenye mnada au kwa njia zingine. Kwa hivyo, ukifuta agizo, ni lazima ulipe salio pamoja na gharama ambazo zinaweza kutokea.

Q. Je, mnakagua magari kabla ya kuyasafirisha?

Magari yote yanakaguliwa kwa umakini ili kuthibitisha hakuna tofauti baina ya maelezo ya hakika na yale yaliyoko kwenye waraka wa maelezo.

Q. Je, ni vipi naweza kutumia huduma za mnada wa mtandaoni?

Unaweza kutumia kila siku.

Q. Je, kuna njia yoyote ya kupata bei elekezi ya gari ambalo ninafuatilia kwa mnada?

Ndio, taarifa kutoka kwa minada ya karibuni itakuwa chanzo chema cha maelezo. Inajumuisha bei ya magari yaliyouzwa kwa miezi mitatu iliyotangulia.

Q. Je, wafanyakazi wenu wanakagua magari kabla ya kuyatilia zabuni kwenye mnada?

Tunao wataalamu wenye ujuzi mwingi ambao ukagua magari. Kabla ya wataalamu waamue kuwekea gari zabuni, wanahakikisha kuwa maelezo ya hakika na hali ya gari yako sambamba na maelezo yaliyotolewa na jumba la mnada.

Kwa maswali zaidi, kuwa huru kuwasiliana nasi

Simu:   +81-45-290-9485
Faksi:  +81-45-290-9486
Barua pepe:   csd@sbtjapan.com