• Nyumbani >
  • Maelezo kuhusu kuuza nje ya nchi

Maelezo kuhusu kuuza nje ya nchi

Yafuatayo ni masharti ya kimsingi ya kibiashara ya SBT:
Bila maelezo yoyote maalum, gari huifadhiwa kwa siku tatu (3) za kazi. Malipo yasio pungua 50% yatahitajika katika muda wa kuhifadhi gari. Kutofuatilia sharti hili agizo la kuhifadhi gari litafutwa mara moja.
Kusafirisha shehena kutaanza maramoja tutakapopokea malipo ya amana ulioweka kulingana na maafikiano ya mteja (wewe) na SBT (sisi).
Punde tutakapopokea malipo kamili, tutakutumia nyaraka zote kupitia kampuni ya uchukuzi wa vifurushi (DHL,FedEx).
Tutapokea Barua za Mikopo (Letters of Credit) kutoka kwa mataifa yaliyochaguliwa.
Nakala ya TT iliyo skaniwa itahitajika baada ya malipo ili kuepukana na kuchelewa kwa kusafirisha shehena au kutayarisha nyaraka.
・Masharti ya kusafirisha shehena:

FOB: Free - On - Board (Bei kabla ya shehena):
Bei ya gari bila kujumuisha uchukuzi wa baharini.Ukinunua gari kwa bei ya FOB, bei inajumuisha bei ya gari na gharama zingine mpaka kuingia melini Japani.
CFR: Cost and Freight.
CIF: Cost, Insurance and Freight.
Bei ya gari ikijumuisha gharama zote zilizotumika Japani pamoja na uchukuzi wa baharini. Kama unahitaji bima kwa gari lako, tafadhali uliza usaidizi.
T.T: Telegraphic transfer / Wire transfer:
Hii ndio njia nzuri zaidi ya kulipa. Ndio ya haraka zaidi, yenye usalama na ya kutegemewa zaidi. Unaweza kutuma pesa kupitia Telegraphic Transfer kwa karibu benki zote maarufu.
L/C: Barua ya Mkopo (Letter of Credit):
Tunapokea Barua za Mkopo (Letters of Credit) kwa mataifa yaliyochaguliwa. Tafadhali wasiliana na benki yako kuhusu nyaraka.